Siku 100 za Utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan

 



Samia Hassan

Siku 100 za Rais Samia Suluhu: Mfahamu Samia Suluhu HaMama Samia Suluhu Hassan ni rais wa sita wa Tanzania ambaye ameingia madarakani Machi 2021 baada ya kifo cha mtangulizi wake John Pombe Magufuli. Alikuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015.

Samia atashikilia wadhifa wa urais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

Ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu zaidi nchini Tanzania. Pia anakuwa rais wa pili wa Tanzania kutokea Zanzibar, wa kwanza akiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 10 kutoka mwaka 1985 mpaka 1995.

Aina ya kuchukua hatamu kwa Samia kumekuja kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, yaani kwa rais kufariki akiwa madarakani na makamu wake kuchukua nafasi.ssan, Rais wa sita Tanzania






Comments