Mashindano ya Olimpiki Tokyo: Mwanariadha wa Nambia anasema 'huwezi kuniambia kwamba mimi sio mwanamke'
Mwanariadha wa Namibia Beatrice Masilingi anajiandaa kushiriki katika mashindano makubwa duniani.
Beatrice mwenye umri wa miaka 18 anasema kwamba anafurahia kushiriki katika mbio za mita 200 upande wa akina dada katika mashindano ya Olimpiki ya 2020 yanayofanyika mjini Tokyo ambapo mbio za kufuzu kwa fainali zitaanza siku ya Jumatatu.
Lakini mbio hizo ni chaguo lake la pili na alikuwa anajiandaa kushiriki mbio za mita 400 ambapo alikuwa miongoni mwa wanariadha wanaopigiwa upatu baada ya kuweka muda bora zaidi mwaka huu wa sekunde 49.53.
Furaha yake katika mashindano ya kufuzu kwa Olimpiki hatahivyo ilikatizwa wakati alipoambiwa na shirikisho la riadha duniani kwamba hangeweza kushiriki katika mbio za mita 400 katika michezo hiyo kutokana na kuwa na viwango vya juu vya homoni za kiume mwilini.
Comments
Post a Comment