Mizozo Nigeria: Fahamu vitisho vitano vya usalama vinavyoikabili Nigeria

 nigeria

Nigeria inakabiliwa na wimbi lisilokuwa la kawaida la mizozo ya kiusalama - kuanzia utekaji nyara hadi wanamgambo wenye msimamo mkali - karibu kila pande ya nchi hiyo imekumbwa na vurugu na uhalifu.

Audu Bulama Bukarti, mchambuzi mwandamizi kuhusu suala la usalama wa Sahel katika Taasisi ya Tony Blair, amesema kiwango cha ukosefu wa usalama kinatishia msingi wa jamii ya Nigeria: "Kwa kila shambulio, maisha ya binadamu yanapotea au kuharibiwa kabisa na imani katika demokrasia nchini humo inapungua".

Wakati Rais Muhammadu Buhari alipochaguliwa mnamo 2015, aliahidi kulinda raia kutokana na magaidi na wahalifu. Lakini ikiwa imesalia chini ya miaka miwili muhula wake madarakani kumalizika,nchi imeendeea kutokuwa na utulivu ikilinganishwa na ilivyokuwa kwa miongo kadhaa. Wengine wamehusisha kuongezeka kwa ukosefu wa usalama hivi karibuni na kiwango cha umaskini mkubwa kote nchini humo. Ukosefu wa ajira kwa vijana kwa sasa hivi ni asilimia 32.5 na nchi iko katika moja ya nyakati mbaya zaidi ya kuporomoka kwa uchumi katika kipindi cha miaka 27 iliyopita.

Comments