“Chanjo ya Corona iwe lazima kwa kila mtu sio hiari” Mbowe (+video)

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe leo ameongea na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza kuhusu Polisi kuzuia kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vijana CHADEMA kuhusu hitaji la Katiba Mpya ambapo pia mambo mengine aliyoyazungumza ni swala la utoaji wa chanjo ya covid-19 kwa Watanzania akimuomba Rais Samia afanye swala la chanjo hiyo kuwa lazima na sio hiyari.

“Serikali inasema chanjo ya Covid-19 ni hiari ya Mtu….. Mtu akatayependa ndiye apewe, huu sio utaratibu wa WHO, Nchi za Wenzetu chanjo ni lazima, tunamuomba Mama Samia aweke utaratibu wa chanjo kuwa lazima na inapaswa itolewe kwa kila Mtu, huu ugonjwa unaua”

”Mgonjwa wa Covid-19 ukilazwa gharama ni zaidi ya Tsh. Milioni 10 kwa wiki mbili, nimeuguza Ndugu yangu Hospitali pale Moshi gharama ni kubwa, kwa siku anatumia mitungi minne kila mtungi ni Elfu 30, ni Watanzania wangapi wanamudu?, gharama zinapaswa kubebwa na Serikali kwakuwa WHO imetangaza kuwa huu ugonjwa ni janga la Taifa” ——— Freeman Mbowe


Comments