- Get link
- X
- Other Apps
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wa bandari ya Bagamoyo pamoja na kufufua mradi wa makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma kwa kuwa soko la chuma kwa Dunia limepanda.
Kauli hiyo ameitoa mkoani Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara.
“Kuhusu bandari ya Bagamoyo tumeanza mazungumzo ya kufufua mradi wote ule wa Bagamoyo pamoja na Mchuchuma na Liganga nilishatoa maelekezo nadhani sekta husika zinaendelea na mazungumzo kuona tatizo ni nini” Rais Samia
“Kuhusu Mchuchuma na Liganga mazungumza yanaendelea kuona tatizo ni nini serikali inaweza kujitoa mpaka wapi, mwekezaji ajitoe mpaka wapi na taarifa zilizopo Duniani chuma imepanda bei ni wakati mzuri wa kuharakisha na kufanya ule mradi” Rais Samia
Comments
Post a Comment