RIPOTI: Matumizi ya bangi yameongezeka mara nne

 


Ripoti mpya iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu UNODC imeonya kwamba idadi ya watu wanaotumia mihadarati duniani inaongezeka na kwamba mwaka jana 2020 pekee duniani kote takriban watu Milioni 275 walitumia mihadarati, hilo likiwa ni ongezeko la asilimia 22 tangu mwaka 2010.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti wa ofisi hiyo ambao pia unatoa mtazamo wa jumla wa soko la mihadarati duniani pamoja na athari zake kwa afya za watu na maisha yao katika mtazamo wa janga la corona.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya dawa za kulevya ya dunia ya UNODC 2021, matumizi ya bangi yameongezeka mara nne katika baadhi ya sehemu za dunia zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Pengo hili la mtazamo bado lipo licha ya ushahidi kwamba matumizi ya bangi yanahusishwa na aina mbalimbali za athari za afya na madhara mengine, hasa kati ya watumiaji wa muda mrefu.

Aidha, nchi nyingi zimeelezea kuongezeka kwa matumizi ya bangi wakati wa janga la COVID-19.

“Mtazamo wa chini wa hatari ya matumizi ya madawa ya kulevya umehusishwa na viwango vya juu vya matumizi ya dawa hizo, matokeo ya ripoti ya dawa za kulevya ya dunia ya UNODC ya 2021 yanaonyesha haja ya kuziba pengo kati ya mtazamo na hali halisi kwa kuelimisha vijana na kulinda afya ya umma,” Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC Ghada Waly.

Comments