Nikki Minaj amtupa mbali Miley Cyrus kwa kuvunja record ya Vevo kupitia video yake mpya ya wimbo wa "Anakonda" baada ya kupata views nyingi ndani ya masaa 24.
Kampuni inayotoa huduma ya kusimamia video "Vevo" imetoa ripoti kuwa video yenye utata ya nikki minaj "Anaconda" rasmi imevunja rekodi ya video iliyotizamwa sana ndani ya masaa 24 iliyokuwa imewekwa na video ya Miley Cyrus "Wrecking Ball"
Vevo walituma tweet leo hii wakisema "Anaconda" imeangaliwa mara milioni 19.6 ndani ya masaa 24 ya mwanzo
Video ya Cyrus "Wrecking Ball,"ambayo ilikuwa inashikilia record hiyo tangu alipoiachia mwaka jana mwezi wa tisa, ilikuwa imeangaliwa mara milioni 19.3 ndani ya masaa 24 ya mwanzo. ni ushindi mdogo kutoka kwa Nikki, lakini bado unaitwa ni ushindi.
Comments
Post a Comment