Kuhusu idadi ya kushtua ya watoto wanaokimbizwa hospitalini kutokana na ulevi wa kupindukia.

mshtuko
Watoto wawili wenye umri wa chini ya miaka 11 wanakimbizwa hospitalini kila wiki kutokana na matatizo ya ulevi wa kupindukia kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo nchini Uingereza.
Idadi ya kushtua ya watoto 102 walifikishwa katika hospitali ya A&E kutokana na kunywa pombe kupita kiasi kwa mwaka jana pekee.
mshtuko2
Hao ni kati ya watoto 2,084 walio chini ya umri wa miaka 15 wanaopelekwa katika vitengo vya dharura kutokana na matatizo yanayohusiana na ulevi wa kupindukia.
Mapema mwaka huu, ilibainishwa kuwa watoto wenye umri wa chini ya miaka minne ni kati ya mamia ya vijana wadogo wanaopelekwa kwa wataalamu wa afya kupatiwa matibabu wakihusishwa na matumizi ya dawa za kulevya na pombe.

Comments