Huyu ndio msanii mwingine kutoka Tanzania anaeshiriki Coke Studio 2014
Kama unakumbuka mwaka jana Diamond Platnumz alishiriki katika kipindi
cha TV cha Coke Studio akiwa pamoja na victoria kimani kutoka kenya na
wasanii wengine kutoka Africa.
Mwaka huu wametoka wasanii watatu watakao shiriki Coke Studio akiwemo
Vanessa Mdee, Diamond pamoja na Joe Makini kutoka Weusi... Joe makini
ameongea ...... msikilize zaidi hapo chini
"hizo taarifanilipigiwa simu sasa hivi nafkiri a week imeisha toka
nimetaarifiwa, nilipigiwa simu kwanza tukaongea, halafu taratibu za
kwenda nairobi zikaanza toka jumatatu na naondoka jumapili na ndege ya
saa nne za asubuhi.
Naichukulia kama moja kati ya hatua nzuru tunazopiga kama joe makini
Weusi na kama watanzania kwasababu hii platform yakekidogo nikubwa
tofauti na show ambazo nimekuwa nikifanya, kwahivyo naichukulia kama
nafasi nyingine nzuri kubwa ambayo mwenyezi mungu amenipa na ambayo
natakiwa niitumie vizuri ili niweze kupiga stepp nyingine kubwa zaidi.
Nitaenda mimi na G Nako kwasababu nimepewa nafasi ya kwenda na mtu mmoja
tu, so G ni mtu ambaye nafanya nae vitu vingi mara nyingi so akiwa
pembeni vitu vingi vinakuwa ni rahisi?

Comments
Post a Comment