
Unaambiwa Matumizi ya Bangi kama kiburudisho yamehalalishwa kutumika kwenye jimbo la Washington nchini Marekani.
Washington ni jimbo la pili nchini Marekani kuhalalisha Bangi baada
ya Colorado ambako jimbo hilo linajipatia mamilioni ya dola kila mwezi
kwa ushuru unaokusanywa kwa biashara za Bangi kwa wanaoitumia
kujiburudisha.

Kwa
sasa ni maduka 25 pekee yaliyoruhusiwa kuuza Bangi ingawa wadau
wanaamini kuwa idadi ya maduka huenda ikaongezaka na kufika miamoja
katika sehemu zingine za Marekani, majimbo 23 yanaruhusu matumizi ya
Bangi kwa sababu za kimatibabu.
Comments
Post a Comment