Msanii muigizaji kutoka Kenya Lupita
Nyong'o ameteuliwa kuijiunga na mabingwa wengine wa kimataifa katika
filamu maarufu zaidi duniani STAR WARS.
Lupita Nyong'o kung'aa zaidi
Lupita
anatarajiwa kuonekana katika kipindi cha saba msimu huu wa Star Wars.
Hii inafatia ufanisi mkubwa aliopata katika filamu '12 years a slave',
ambapo alinyakua taji la Oscars la muigizaji bora msaidizi.
Gwendoline Christie
Msanii mwingine aliyetajwa kujiunga na 'star
Wars' ni Gwendoline Christie,ambaye kwa sasa anatambulika zaidi katika
mchezo wa televisheni wa 'Game of Thrones' unao endelea kupata umarufu
duniani. Yeye pia ataonekana katika filamu ya 'Hunger Games'."Nashindwa kuelezea furaha yangu kwa Lupita na Gwendoline kwa kujiunga na waigizaji wengine katika kipindi hiki cha Star Wars.,'' amesema Kathleen Kennedy, rais wa kampuni ya Lucasfilm inayosimamia utengezajiwa filamu hiyo.


Comments
Post a Comment