Priince Charles na mkewe Camilla wakiwa katika ziara yao nchini Canada
Naibu balozi wa Urusi mjini London ameomba kukutana
na maafisa wa wizara ya mambo ya nje wa Uingereza kujadili matamshi ya
Mwanamfalme wa Uingereza Prince Charles ambapo amefananisha vitendo vya
Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Ukraine na uliokuwa utawala wa
kinazi nchini Ujerumani chini ya Adolf Hitler.
Prince Charles ambaye yuko kwenye foleni
kumrithi Malkia wa Uingereza , alitoa matamshi yake Jumatano alipokuwa
anazungumza na mfanyakazi mmoja wa Poland katika makavazi ya wahamiaji
eneo la Nova ScotiaWalikuwa wanajadili hatua ya Hitler kunyakua nchi wakati wa utawala wake wakati ambapo mwanamfalme huyo alipofananisha kitendo hicho na kilichofanyika nchini Ukraine kwa maagizo ya Rais Vladimnir Puti.
Prince Charles anatarajiwa kuhudhuria hafla moja nchini Ufaransa mwaka ujao
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, amesema kuwa sio jambo la kawaida mwanamfalme kutoa kauli za kisiasa wakati wa mzungumzo ya faragha na kwamba kwa sasa hawawezi kutamka lolote kuhusu zogo hilo.
Mnamo siku ya Jumatatu, Prince Charles na mkewe Camilla walitembelea makavazi ya kitaifa ya wahamiaji nchini Canada, wakati wa ziara yao ya siku nne nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema kuwa ombi la kufanyika mkutano ni dalili ya Urusi kukasirishwa na matamshi ya Prince Charles ingawa Urusi imejizuia kugeuza swala hilo na kulifanya kuwa mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.
Inaaminika kuwa Urusi inataka ufafanuzi kuhusu matamshi ya Mwanamfalme huyo.
Comments
Post a Comment